Taharuki : NYUKI WAVAMIA WAOMBOLEZAJI NA KUKWAMISHA MAZISHI YA MSANII WA NYIMBO ZA ASILI 'KALANGA'...TAZAMA,PICHA, VIDEO

Katika hali isiyo ya kawaida nyuki wa ajabu wameibuka na kushambulia waombolezaji muda mfupi tu baada ya mwili wa Msanii wa nyimbo za asili maarufu kwa jina la Kalanga "Ng'wana Kolagwa" kufikishwa katika kaburi lake.

Msanii Kalanga alifariki dunia siku ya Jumatano Februari 21,2018 majira ya saa 11 alfajiri nyumbani kwao katika kijiji cha Chambo - Mwamakumbi Nzega mkoani Tabora baada ya kuugua muda mrefu.

Mazishi yamefanyika jana Alhamis Februari 22,2018  nyumbani kwao majira ya saa moja usiku baada ya waombolezaji kushindwa kumzika marehemu saa nane mchana kutokana na kuvamiwa na kundi la nyuki.


Inaelezwa kuwa baada ya mwili wa marehemu kufikishwa katika kaburi kwa ajili ya mazishi,ghafla walitokea nyuki na kuanza kuwashambulia waombolezaji zaidi ya masaa matatu na kusababisha taharuki kubwa kila mmoja akipambana na hali yake kujinusuru na balaa hilo la nyuki. 

Hata hivyo baada ya balaa hilo la zaidi ya saa tatu wazee walifanya tambiko kukabiliana na nyuki ndipo nyuki wakatoweka na kufanikiwa kumzika marehemu.

Mbali na tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina/kichawi ,Wataalamu wa mambo wanasema mila na desturi za uzikaji wa ma manju/wasanii wa nyimbo za asili zilikiukwa.

ANGALIA VIDEO BALAA LA NYUKI MSIBANI 


Msanii Kalanga "Ng'wana Kolagwa" enzi za uhai wake
Mwili wa marehemu Kalanga ukiingizwa kaburini
Waombolezaji wakiondoka kaburini baada ya nyuki kuibuka kaburini
Waombolezaji wakitawanyika
Nyuki balaa...kila mtu anapambana na hali yake....
Mmoja wa waombolezaji akionesha  jinsi mdomo ulivyoshambuliwa na nyuki

ANGALIA HAPA BAADHI YA NYIMBO ZA KALANGA











Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527