TUNDU LISSU AMLILIA KINGUNGE

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia kifo cha Kingunge Ngombale Mwiru akisema historia itamkumbuka.


Akizungumza leo Februari 2, 2018 ameanza kwa kusema “namtakia mapumziko mema.”


Amesema Mzee Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wenye historia kubwa na alionyesha ujasiri mkubwa wa kuhama chama chake cha CCM bila kuhofia kuhudhuriwa kutokana na mazingira yalivyokuwa.


“Ni mmoja wa wazee walioonyesha ujasiri mkubwa katika mazingira ya siasa za Tanzania yalivyokuwa, akahama chama tena CCM bila hofu za kuhudhuriwa akaeleza madhabi yake kuwa hiki chama (CCM) kinatupeleka kuzimu,” amesema Lissu na kuongeza “historia itamkumbuka.”


Kingunge aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba nane, Oktoba 4, 2015 alitangaza kukihama chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote lakini mara kadhaa alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi aliyekuwa mgombea urais wa Chadema/Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527