RAIS MAGUFULI AMSAIDIA BAJAJI MLEMAVU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kumsaidia Bajaj Mlemavu wa viungo Bw. Yusuf Abdulrahaman Ndemanga.


Bw. Ndemanga amekabidhiwa Bajaji hiyo na Katibu waRais Bw. NgusaSamike, Ikulu Jijini Dar es Salaam jana tarehe 02 Februari, 2018.

Mhe. Rais Magufuli alikutanana Bw.Ndemanga tarehe 25 Agosti, 2017 katika sehemu ya abiria wakati akisubiri kupanda kivuko cha MV Magogoni kuelekea Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kukutana na Mhe. Rais Magufuli, Bw. Ndemanga alimuomba msaada wakupatiwa Bajaj iliimsadie kupata kipato.

Akikabidhi msaada huo Bw. Ngusa Samike amemtaka Bw. Ndemanga kuitumia Bajaj hiyo vizuri nakujiongezea kipato kitakacho msaidia yeye na familia yake.

“Mhe. Rais amenituma nikukabidhi Bajaj hii mpya kabisa, matarajio yake nikuwa itakusaidia kupiga hatua za kimaendeleo, anatarajia kukuona unaongeza Bajaj nyingine na unaisaidia familia yako kupata nafuu ya maisha na sio kuja kuomba msaada mwingine” amesema Bw. NgusaSamike.

Kwa upande wake Bw. Ndemanga aliyeongozana na Mkewe Bi. Hawa Mohamed amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa msaada huo na ameahidi kuwa ataitumia Bajaj hiyo vizuri kuzalisha kipato kwa ajili ya familia yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527