Picha 6 : JINSI LOWASSA ALIVYOFIKA NYUMBANI KWA KINGUNGE KUHANI MSIBA


Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema,Mheshimiwa Edward Lowassa akitia sahihi kwenye Kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Kingunge alipowasili jana jioni

Mbali na Lowassa pia walikuwepo viongozi wastaafu wa serikali kama Mzee Pius Msekwa na mkewe Mama Anna Abdalah,Waziri Mkuu wa zamani Mheshimiwa Salimu Ahmed Salimu,na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova.

Kingunge alifariki alfajiri ya jana Ijumaa februari 02, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kutokana na kujeruhiwa na mbwa nyumbani kwake jijini Dar 

Mzee Kingune anatarajiwa kuzikwa Jumatatu 05,2018,katika Makaburi ya Kinondoni Dar es salaam.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527