MWENYEKITI WA MTAA WA BUNGONI ATOA MABATI 150 KUCAHNGIA UJENZI WA ZAHANATI ILALA



Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bungoni Ilala, Barua Mwakilanga akikabidhi bati 150 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, leo jijini Dar es Salaam. Ametoa bati hizo kuitikia wito ulitolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa kumwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchangisha fedha kwa wadau ili kupatikana fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Ilala.

Sophia Mjema akizungumza baada ya kupokea bati hizo
"Bati hizi pelekeni kuzihifahdhi kuleee", Sophia Mjema akiwaelekeza vijana baada ya kupokea bati hizo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Sophia Mjema akizungumza na Waandishi baada ya kupokea mabati hayo. Katikati ni Ndugu Barua. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527