MSAIDIZI WA LISSU : MAHAKAMA SIYO SEHEMU YA MAJARIBIO..WATENDAJI WOTE WAIHESHIMU

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527

Makamu wa Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Godwin Ngwilimi amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na watendaji wote wa sheria kuiheshimu mahakama kwani ni sehemu ambayo ukienda mwishowe haki inapatikana.

Akizungumza jana wakati alipokuwa kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria ambapo ameonya mahakama zisitumike kuonea watu wengine huku akikazia kuwa mahakama haipaswi kuwa sehemu ya majaribio kwani siyo maabara.

"Msiruhusu hata mara moja kwani mnalindwa na Katiba. Msimamie hayo ili mahakama isiendelee kuonekana sehemu ya mchezo mchezo. Maisha ya jamii ni mapana kuliko migogoro au hata sheria. hivyo nadiriki usema kwamba siyo lazima maisha ya jamii ni sheria au ni lazima yaishe kisheria au mahakamani." Tusichukulie Mahakama kama jumba la kamari," Wakili Ngwilimi.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.