Maajabu : MWANAMKE ATUMIA MBEGU ZA KIUME ZA MWANAYE ALIYEFARIKI KUPATA WAJUKUU

Rajashree Patil akiketi karibu na picha ya mwanawe aliyefariki kutokana na saratani ya ubongo.

Miaka miwili ilioipita, Rajashree Patil alipoteza mwanawe wa miaka 27 aliyefariki kutokana na saratani ya ubongo.

Huku akipata changamoto za kuweza kuishi bila mwanawe Rajashree alitumia mbegu za kiume za mwanawe ambaye alikuwa hajaoa ziliohifadhiwa ili kupachika mimba mwanamke mwengine aliyeikuza.

Hatua hiyo ilifanikiwa na mama aliyepachikwa mimba hiyo akajifungua pacha. Rajshree amemtaja mmoja wa pacha hao jina la mwanawe.

Hiki ni kisa kisichokuwa cha kawaida cha mwalimu mwenye umri wa miaka 49 kutoka India ambaye alikabiliana na changamoto za kila aina ili kutomsahau mwanawe aliyefariki akiwa na umri wa miaka 27 kutokana na saratani.

Akisaidiwa na mama aliyekubali kupachikwa mimba hiyo kwa lengo la kulipwa mwanamke huyo alifanikiwa kupata watoto wawili mmoja akiwa mvulana na mwengine msichana.

Anasema kuwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa mwanawe anaishi. Baada ya kufuzu kutoka chuo cha uhandisi cha Sinhgad mjini Pune, Mwanawe Rajshree Prathamesh alielekea mjini Ujerumani 2010 kusomea shahada.Prathamesh alipatikana na uvimbe katika uboingo wake 2013 na kufariki miaka mitatu baadaye.

Mwaka 2013, alipatikana na uvimbe wa ubongo na kufariki 2016 lakini mbegu zake za kiume zilihifadhiwa na baadaye kutumika kumpachika mama wa mimba za biashara aliyejifungua pacha hao.

''Nimempata mwanangu Pramesh'', mamake Rajashree Patil aliambia BBC.

''Nilimpenda sana mwanangu, alikuwa mwerevu sana shuleni na alikuwa akisomea shahada katika uhandisi nchini UJerumani alipopatikana na uvimbe huo ikiwa ni awamu ya nne ya saratanii katika ubongo.

Madaktari walikuwa wamemwambia Pramesh kuhifadhi shahawa yake kabla ya kuanza matibabu ya kutumia kemikali na miale, alisema.

Prathamesh ambaye alikuwa hajaoa alikuwa amemchagua mamake na dadake Dnyanashree kutumia shahawa hiyo baada ya kifo chake.Pacha Prathamesh na Preesha

Wakati huo bi Rajshree hakubaini kwamba hiyo itakuwa njia ya kumpata mwanawe.

Shahawa hiyo iliohifadhiwa ilichanganywa na yai ambalo halijaulikani mwenyewe na kupachikwa kwa kizazi cha mwanamke anayefanya biashara ya kukuza mimba.

Baada ya mwanawe mwenye umri wa miaka 27 kufariki kutokana na saratani ya ubongo miaka miwili iliopita, Rajshree alikataa kuomboleza na badala yake alitumia shahawa hiyo ya mwanawe kupata wajukuu hao.

Pacha hao walizaliwa februari 12 na Rajshree aliwapatia majina ya Prathamesh baada ya jia la mwanawe na Preesha (zawadi ya mungu).
Dr Supriya Puranik, ni mtaalam wa mfumo wa IVF katika hospitali ya Sahyadri

Huku akisukumwa na lengo la kumpata mwanawe Dr Supriya Puranik, ambaye ni mtaalamu wa IVF katika hopsitali ya Sahyadri alisema mbinu ya IVF ilikuwa kitu cha kawaida lakina kisa hiki kilikuwa cha kipekee kwa kuwa mama aliyekuwa na huzuni alitaka kumpata mwanawe kwa gharama yoyote ile.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527