BAM INTERNATIONAL YAWAPA SAPOTI WATOTO YATIMA KIMARA DAR ES SALAAM


Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya BAM International Noreen Mazalla (wa pili kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mlezi wa ‘New Hope for Girls Organization’ Consoler Wilbort kwenye makazi ya watoto takribani 38 wa kike mayatima wanaolelewa na familia hiyo Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. Kampuni ya Ujenzi ya Bam International imetoa pia msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu kwa familia hiyo. Anayeshuhudia (nyuma kushoto) ni Meneja Kambi na Majengo ya Kampuni hiyo, Wim Mulderij. (Picha na Robert Okanda Blogs)
Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya BAM International Noreen Mazalla (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa watoto, Loveness Julius (kulia) na Rechol Lazaro wanaolelewa kwenye makazi ya ‘New Hope for Girls Organization’ Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. Kampuni ya Ujenzi ya Bam International imetoa pia msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu kwa watoto takribani 38 wa kike mayatima wanaolelewa na familia hiyo. Anayeshuhudia (wa pili kushoto) ni Meneja Kambi na Majengo ya Kampuni hiyo, Wim Mulderij.
Meneja Kambi na Majengo ya Kampuni Kampuni ya BAM International, Wim Mulderij akigawa dawa za mswaki kwa sehemu ya watoto takribani 38 wa kike mayatima wanaolelewa ‘New Hope for Girls Organization’ Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. Kampuni ya Ujenzi ya Bam International imetoa pia msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu kwa familia hiyo. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni hiyo, Noreen Mazalla.
Mlezi wa ‘New Hope for Girls Organization’ Consoler Wilbort (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya BAM International Noreen Mazalla wakati wa hafla hiyo, Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana.
Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya BAM International Noreen Mazalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoto takribani 38 wa kike mayatima wanaolelewa ‘New Hope for Girls Organization’ Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. Kampuni ya Ujenzi ya Bam International imetoa pia msaada wa vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu kwa familia hiyo. Pamoja nao (nyuma kushoto) ni Meneja Kambi na Majengo ya Kampuni hiyo, Wim Mulderij.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527