WAZIRI JAFO AWAONYA WAKURUGENZI NA WAKUU WA WILAYA KUWEKA SIRI ZA SERIKALI WHATSAPP

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri (DED) kutunza siri za Serikali.


Jafo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Januari 29,2018 mjini Dodoma alipofungua mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mikoa sita.


Mafunzo hayo ni mwendelezo wa ambayo yanatolewa kwa viongozi wa kada hiyo.


Waziri Jafo amesema ujenzi wa Serikali utakuwa mzuri iwapo viongozi hao watakuwa makini na kutunza siri.


"Hivi unakuwaje wewe mkurugenzi au mkuu wa wilaya unapeleka siri za Serikali kwenye mitandao ya kijamii na nyingi unaziona kwenye WhatsApp, inatia aibu sana," amesema Jafo.


Amewataka wakurugenzi kujipambanua na kusimamia miradi ya maendeleo katika kukusanya mapato na kuyatumia vyema na hasa ya ndani.


Jafo amesema tatizo kubwa kwa wakurugenzi ni kutofanya uamuzi kwa haraka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527