WANANCHI WA GAIRO WAFURAHIA UJENZI WA BARABARA YA LAMI


Mkuu wa Wilaya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (aliyevaa kiti jekundu la drafti) akimuonyesha Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Shabiby madhara ya miundombinu kwa mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani humo
Mkuu wa Wilaya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (aliyevaa kiti jekundu la drafti) akimuonyesha Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Shabiby madhara ya miundombinu kwa mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani humo.
Mbunge wa Gairo, Mhe. Ahmed Shabiby, akielezea hali ya barabara kwasasa na jinsi ilivyokuwa zamani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bi. Agnes Mkandya akifafanua jambo.
Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro, Kilian akielezea jambo mbele ya viongozi wa wilaya ya Gairo walifika kutembelea barabara hiyo kujionea eneo lililoadhiriwa na mvua.

Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania (TARURA), Gairo Bw. Simon akielezea jambo wakati wa ziara hiyo. Pembeni kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe na (wa kwanza kulia) ni Mbunge wa Gairo, Mhe. Ahmed Shabiby wakiwa na viongozi wengine.

****
Wananchi wa Wilaya ya Gairo wametoa shukrani zao za pekee kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuwawezesha kupata barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 3.5.

Hayo yamezungumzwa na Kata ya Magoweko mwishoni mwa wiki hii wakati wa ziara ya viongozi wa wilaya ya Gairo walipofanya ukaguzi wa barabara hiyo ambayo kwa sasa ipo hatua za mwisho kumalizika.

"Wana Gairo tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwani barabara ya lami ni muujiza hatukuwahi kuota kama itatokea," walisema wakazi hao.

Viongozi hao ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe, Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Shabiby, Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Bw. Shabani Sajilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Meneja TARURA. Bw. Simon, Wajumbe KUU (W) nk walifanya ziara hiyo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea Wilayani.

Aidha dhumuni rasmi la ukaguzi huo ilikuwa ni kuhakikisha ujenzi huo unaisha kwa wakati ambapo barabara inatakiwa kukabidhiwa Januari mwaka huu.

Barabara hiyo ni matokeo ya ahadi ya aliyekuwa Waziri wa Ujenzi ambaye kwa sasa ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Gairo miaka mitatu iliyopita kwenye mkutano wa hadhara ambao Mgeni Rasmi alikuwa rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527