WAGOMBEA 27 WA UBUNGE NA UDIWANI WATEULIWA KUGOMBEA UCHAGUZI MDOGO

Wagombea 27 wa ubunge na udiwani wameteuliwa kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Februari 17, mwaka huu katika majimbo mawili ya ubunge na kata nne.

Katika uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, mgombea udiwani kupitita CCM katika kata ya Kimagai iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, amepita bila kupingwa.

Mbali na uteuzi huo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika kata sita za Tanzania Bara wanatarajia kuteua wagombea wa udiwani wa kata hizo siku ya Jumatano ya tarehe 24 Januari, 2018 kukamilisha kata 10 zilizopangwa kushiriki Uchaguzi Mdogo wa Februari 17, 2018.

Akizungumzi uteuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Hamis Mkunga amesema mgombea huyo wa CCMa amepita bila kupingwa baada ya mgombea wa CHADEMA kushindwa kurejesha fomu za uteuzi.

Amesema katika uteuzi wa wagombea Jimbo la Kinondoni, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo amewateua wagombea 12 ambao ni ambao ni Godfrey Maliza kutoka chama cha TLP, Johnson Mwangosya (SAU) na Mwajuma Milambo kutoka UMD.

Mkunga amewataja wagombea wengine walioteuliwa kuwa ni John January Mboya (Demokrasia Makini), Maulidi Mtulia (CCM), na Mary Mpangala wa DP.

Wengine ni Salim Mwalimu (CHADEMA), Rajabu Salum (CUF), Mohamed Majaliwa (NRA), George Christian (CCK), Ally Omari Abdallah (ADA THADEA) na Ashiri Kiwendu wa AFP

Kuhusu uteuzi wa wagombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, Mkunga amewataja wagombea wanne walioteuliwa kuwa ni Dk Godwin Mollel (CCM) Mdoe Azania Yambazi (SAU), Tumsifuheri Mwanry (CUF) naElvis Christopher MosiwaCHADEMA.

Katika kata tatu zilizobaki, Mkunga amevitaja vyama vya siasa vilivyopitisha wagombea ambao waliteuliwa katika kata ya Isamilo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza kuwa ni Chama cha CUF, DP, UDP, CCM, na CHADEMA.

Amevikumbusha vyama na wagombea kuheshimu maadili ya uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni kwani vyama vyote vimekubaliana kuheshimu maadili hayo na kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingisiku ya kupiga tarehe 17 Februari mwaka 2018.

Na Hussein Makame-NEC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527