SERIKALI YALIFUNGA KANISA LA MHUBIRI MTATA 'ANAYETEMBEA ANGANI' NA FEDHA ZA MIUJIZA


Serikali ya Botswana imelifunga kanisa la muhibiri mmoja wa Malawi mwenye utata anayedaiwa ''kutembea angani''.

Serikali ilithibitisha kufungwa kwa kanisa la Bushiri la Christian Gathering Church ECG mjini Gaborone mara kadhaa kutokana na wasiwasi kuhusu ''fedha za miujiza''.

Chombo cha habari cha Malawi24 kimeripoti kwamba kanisa hilo lilipinga uamuzi huo mahakamani uliochukuliwa chini ya mwaka mmoja baada ya muhibiri huyo kupigwa marufuku kuingia nchini humo.

Alikuwa ametarajiwa kuhudhuria kongamano fulani.
Mhubiri Bushiri wa kanisa la Christian Gathering Church ECG mjini Gaborone

Hata hivyo waziri wa Botswana Edwin Batshu alitangaza mnamo mwezi Aprili 2017 kwamba bwana Bashir ambaye sasa anaishi Afrika Kusini atahitaji Visa ili kuingia, licha ya raia wa Malawi kutohitaji kibali hicho kulingana na chombo cha habari cha AllAfrica.com

Serikali imetangaza kwamba kanisa hilo litafungwa kabisa, huku gazeti hilo la Botwana likipata barua ilioambia usimamizi wake kwamba kibali cha kuendesha kanisa hilo kimefutiliwa mbali.

Gazeti hilo limeongezea kwamba ni hatua ya kanisa hilo kutumia ''fedha za miujiza'' ambayo imevunja sheria za taifa hilo.

Bwana Bushiri ambaye ana zaidi ya ''likes'' milioni 2.3 katika mtandao wa facebook na ambaye alivutia umati mkubwa wa kuweza kujaza uwanja wa FNB mkesha wa mwaka mpya bado hajatoa tamko lolote.

Kanisa hilo ni maarufu kwa mtindo wake wa maisha ya kifahari kutokana na ufanisi wake ambao umevutia wafuasi wengi barani Afrika.

Alishutumiwa mwaka uliopita baada ya kubainika alikuwa akiwatoza kati ya dola 80 hadi 2000 wafuasi wake waliotaka kuhudhuria chakula cha jioni naye kulingana na chombo cha habari cha Afrika Kusini South Africa News24.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527