MWANASAYANSI JOHN YOUNG ALIYETEMBELEA MWEZINI MARA KADHAA AMEFARIKI DUNIA

John Young alifanya safari yake ya kwanza na Gemini 3 mwaka 1965


Mwanasayansi wa safari za anga za juu raia wa Marekani John Young ambaye alisafiri kwenda mwezi mara mbili na kuhudumu kama kamanda ya chombo cha kwanza cha safari za anga za juu amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.

Young alikuwa mtu pekee kuwahi kushiriki safari za anga za juu za Gemini, Apollo na Space Shuttle.

Wakati mmoja pia alipata umaarufu kwa kusafirisha kisiri nyama kwenda safari ya anga za juu kwa mwanasayansi mwenzake kama zawadi.John Young, kulia, alikuwa rubani wa chombo cha kwanza mwaka 1981

Young alistaafu mwaka 2004 baada ya taaluma ya miaka 42. Nasa wanasema kuwa alifariki siku ya Ijumaa kutokana na ugonjwa wa kichomi.

Baada ya kuzaliwa huko San Francisco mwaka 1930 alipata shahada ya uandisi kutoka taasisi ya Georgia Institute of Technology na baadaye kuhudumu kama rubani wa jeshi la wanamaji wa Marekani.Young, katikati, alishiriki katika safari ya Apollo 10

Alijiunga na Nasa mwaka 1992 na mara ya kwanza kusafiri kwenda anga za juu mwaka 1965 wakati wa safari ya Gemini 3.

Mwezi Mei mwaka 1969 Young alikuwa miongoni mwa wanasayasansi waliosafiri kwa chombo cha Apollo 10 kama jaribio la safari ya kwenda mwezini kwa chombo cha Apollo 11 miezi miwili baadaye

Young baadaye alitembea kwa miguu mwezini mwaka 1972 kama kamanda wa safari ya Apollo 16.John Young ametajwa na Nasa kama mwanayasanyi mwenmye ujuzi wa juu zaidi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527