MSUKUMA AWAPA MAKAVU CHADEMA...ASEMA HAWANA UBAVU WA KUMFUKUZA LOWASSA

Mbunge wa Geita, Joseph Msukuma amesema kwamba viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wanapiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Lowassa kwenda Ikulu lakini hawana mabavu ya kumfukuza uanachama kwani yeye ndiye mwenye chama.


Msukuma amedai kwamba, Mbowe ambaye anaaminiwa kuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA tayari alikwishauza chama kwa Lowassa muda mrefu ndiyo maana hana sauti ya kumuwajibisha.


Aidha Msukuma hajaishia hapo ambapo pia amemtaka Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho aoneshe nguvu yake ndani ya chama kwa kumwambia Lowassa aombe radhi na siyo waombane wao kwa wao kwani kutakuwa ni kuwapumbaza wanachama na wafusi wao bali hadharani watu waone.


"Lowassa ndiye mwenye Chama. Wewe mbowe uliuza chama sasa wewe kama msemaji toa kauli ya kumfukuza chama Lowassa. Tunashangaa kuanza kuchafuliwa kwa mtu ambaye mlituaminisha kuwa anafaa kuwa Rais. Muite Lowassa umhoji mitandaoni tuone akikuomba radhi. Na hata akikuomba radhi sasa hivi tutajua siyo kwa mapenzi yake," Msukuma.


Ameongeza kuwa, "Mbowe kusema kuwa Lowassa alikurupuka ni kumkosea adabu kwanza, Lowassa ni mtu mzima kwake na yeye bado ni kijana. Na ninaamini kwamba wewe Mbowe Lowassa hakuombi msamaha kwa kuwa yeye ndiye mmiliki".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527