MSANII ALIYEFUNGIWA KWA PICHA ZA UCHI AOMBA RADHI

Msanii filamu na video vixen, Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind amefunguka na kuomba radhi kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kutokana na vitendo vyake vya kupiga na kuweka picha mitandaoni za nusu uchi.


Akiongea jana na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungiwa na serikali kujihusisha kufanya kazi zozote za sanaa kwa miezi sita, Pretty Kind alisema kuwa amejifunza na kugundua kuwa alikuwa anafanya makosa hivyo sasa hataweza kurudi tena kufanya mambo hayo.


“Naomba niombe radhi kwa Watanzania wote kwa hiki nilichokifanya natambua nimefanya kosa naomba msamaha aweze kunisamehe, pia naomba msamaha kwa mashabiki zangu kwa hiki kilichotokea nimejifunza hivyo nitakuwa Pretty Kind mwingine mpya na kufanya yale yanayotakiwa katika jamii” alisema


Pretty Kind amefungiwa kujihusisha na sanaa kwa takribani miezi sita baada ya kuposti picha katika mtandao wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa nusu utupu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Kitanzania na kwenda kinyume na maagizo ya Rais John Pombe Magufuli ambayo aliyatoa hivi karibuni kuwataka wasanii wa kike kuvaa kwa staha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527