Makubwa haya ! AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUBAKA MBUZI WAWILI KISHA KUWAUA

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527

Mtu mmoja nchini Kenya mwenye umri wa miaka 35 amefikishwa mahakamani akituhumiwa kubaka mbuzi wawili wa jirani yake, na kisha kuwaua.


Tukio hilo limetokea Januari 13 mwaka huu, baada ya watu kumuona akiwaburuza mbuzi hao kutoka porini ambako anahisiwa kufanya tukio hilo, katika eneo la Kangundo


Waendesha mashtaka wametaka mbuzi hao wapelekwe kufanyiwa vipimo ili kubaini kama kweli wamefanyiwa kitendo hicho, na kutaka mshtakiwa kupatiwa matibabu baada ya kulalamika alipigwa vibaya na polisi walipoenda kumkamata.


Kesi hiyo imehairishwa mpaka Januari 29, na mshtakiwa kupewa dhamana ya shilingi 100,000 za Kenya.


Sheria za Kenya zinamtaka mtu atakayekutwa na hatia ya kufanya ukatili kama huo kwa wanyama kwenda jela kwa miaka 14.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.