MAJINA YA SHULE 10 BORA, 10 ZA MWISHO MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017...ANGALIA MATOKEO YOTE HAPA


Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba. Shule  iliyoshika namba moja inatoka Mbeya.


Jumla ya watahiniwa  385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.



Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.

"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.

Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani  matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.

SHULE 10 BORA.

1. St. Francis Girls ya Mbeya



2. Feza Boys ya Dar es salaam


3. Kemebos ya Kagera 

4. Bethel Sabs Girls ya Iringa 

5. Anwarite Girls ya Kilimanjaro 

6. Marian Girls Pwani 

7. Canossa ya Dar es salaam 

8. Feza Girls ya Dar es salaam 

9. Marian Boys ya Pwani 

10. Shamsiye Boys ya Dar es salaam 

SHULE 10 ZA MWISHO KITAIFA
10. Mtule ya Kusini Unguja

9. Nyeburu ya Dar es salaam

8. Chokocho ya Kusini Pemba

7. Kabugaro ya Kagera

6. Mbesa ya Ruvuma

5. Furaha ya Dar es salaam

4. Langoni ya Mjini Magharibi

3. Mwenge S.M.Z ya Mjini Magharibi

2. Pwani Mchangani ya Kaskazini Unguja

1. Kusini ya Kusini Unguja

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527