MADIWANI WENGINE WA CHADEMA ARUSHA WAHAMIA CCM



Madiwani watatu wa Chadema, katika halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha , wametangaza kujiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ( CCM).

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Longido, Jumaa Mhina alithibitisha leo Januari 10 kujiuzulu kwa madiwani hao, Jacob Silas Mollel Kata ya Elang'atadapash, Elias Mepukori Mbao Kata ya Kamwaga na Diyoo Lomayani Laizer Kata ya Olmolog.


Mhina amesema sababu za kujiuzulu madiwani hao wamezitoa kuwa ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi, kuinua uchumi na pia kurejesha nidhamu kazini.


"Tayari tumepokea barua zao na tumezipeleka TAMISEMI kwa ajili ya utaratibu wa kisheria ili kuwezesha kufanyika uchaguzi mdogo baada ya Tume kupata taarifa" Amesema


Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido, Onesmo ole Nangole pia amethibitisha kuondoka kwa madiwani hao na kueleza chama hicho, kinafuatilia tukio hilo.


Madiwani hao kujiunga na CCM wanafanya mkoa wa Arusha pekee kuwa na jumla ya madiwani 13 wa Chadema ambao wamejiuzulu na kujiunga na CCM tangu kumalizika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Na Mussa Juma, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527