KINGUNGE AREJESHWA MUHIMBILI KUENDELEA NA MATIBABU

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru amerejeshwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuendelea na matibabu.


Kingunge aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo Januri 10, 2018 ili kwenda kushiriki tukio la mazishi ya mkewe ,Peras Ngombare Mwiru yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kinondonbi jijini Dar es Salaam.


Pares alifariki dunia Januari 4, katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa ugonjwa wa kupooza huku Kingunge naye akilazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake, Victoria jijini humo hivi karibuni.


Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombare Mwiru jana alisema baada ya baba yake kupata kumzika mkewe amerejea hospitalini ili kuendelea na matibabu kama alivyotakiwa na madaktari wake.


“Leo (jana) Mzee (Kingunge) amerudishwa hospitalini tayari kwa ajili ya kuendelea na matibabu na amelazwa ICU (chumba cha wagonjwa mahututi) cha Mwaisela na hali yake inaendelea vizuri,” alisema Kinje.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527