STEVE NYERERE AANIKA UGONJWA UNAOMSUMBUA

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527Msanii wa filamu, Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa ana wiki mbili yupo kitandani na kwamba ugonjwa unaomsumbua ni nyama kushikana na mifupa.

Amesema ugonjwa huo umemsababisha kushindwa kufanya kazi yoyote na kushindwa kutembea.

Muigizaji huyo amekiambia kipindi cha Enewz ya EATV kuwa anashangaa kwanini kila mtu anaongea lake kuhusu kuumwa kwake huku wengine wakifika mbali zaidi kwa kudai kwamba ameathirika.

“Watu wananifuatilia kutaka kujua hali yangu kwa sababu mimi ni mtu maarufu, ni jambo jema lakini kama kuna watu wamenitupia vitu vya ajabu naomba wanisamehe, mimi ni binadamu labda kuna namna watu nimewakosea,” amesema Steve. 

“Lakini nashangaa kuna watu wanadai imeathirika mmenipima, yaani kila mtu anaongea lake,”

Theme images by rion819. Powered by Blogger.