CCM WAIBUKA WASHINDI UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA SONGEA MJINI,SINGIDA KASKAZINI NA LONGIDO



Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mdogo wa marudio wa ubunge katika majimbo ya Songea Mjini, Singida Kaskazini na Longido.


Akitangaza matokeo hayo Singida Kaskazini, msimamizi wa uchaguzi, Rashid Mandoa amemtangaza Justine Monko wa kuwa mshindi baada ya kupata kura 20,857 sawa na asilimia 93.5.


Amesema wagombea wengine na kura walizopata katika mabano ni Dalphine Mlewa wa CUF (974), Aloyce Nduguta wa Ada-Tadea (265), Omar Sombi wa AFP (116) na Mchungaji Yohana Labisu wa CCK kura 86.


Amesema kura zilizopigwa ni 22,298, waliojiandikisha kupigakura ni 91,518, “watu 69,220 ambao ni zaidi ya asilimia 70 hawakujitokeza kupiga kura.”


Katika jimbo la Songea Mjini, msimamizi wa uchaguzi, Tina Sekambo amemtangaza Dk Damas Ndumbaro kuwa mshindi kwa kupata kura 45,762 sawa na asilimia 97.

Amesema Christina Thinangwa wa CUF amepata kura 608 huku Neema Tawete wa ADA-TADEA akipata kura 471 na kubainisha kuwa waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 28,841.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Longido, Jumaa Mhina amemtangaza Dk Stephen Kiruswa kuwa mshindi baada ya kupata kura 41,258 sawa na asilimia 99.1.
Chanzo-Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527