BINTI AJIUA BAADA KUKOSEA KUTUMA MESEJI....MARA PAAAP !! IKAENDA KWA MPENZI BADALA YA RAFIKI YAKE


Binti mmoja nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 17, Charlotte Guy, 17, amejiua kujiua baada ya kukosea kutuma meseji na kwenda kwa mpenzi wake badala ya rafiki yake.

Charlote ambaye alikuwa akimtumia rafiki yake meseji kwa kutumia snapchat akimwambia kuwa amelala na mwanaume mwingine, alikosea kutuma meseji hiyo na kwenda kwa mpenzi wake Jack Hurst mwenye umri wa miaka 20.

Watu wa karibu wa wawili hao wamesema kwamba baada ya kufanya hivyo alimtumia meseji ya kumuomba radhi Jack na kumuaga ikisema ..”Kwa heri, tafadhali nisamehe, nakupenda, lakini kujua kuwa unanichukia inatosha”.

Baada ya hapo Jack alianza kumtafuta kwenye simu mpenzi wake huyo bila mafanikio na kuamua kuita polisi na kwenda chuoni kwao kumtafuta, na kukuta amejinyonga karibu na eneo la chuo alichokuwa akisomea masuala ya afya.
Jack Hurst ambaye ni mpenzi wa Charlote

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527