BASI LA KAMPUNI YA TAHMEED LATEKETEA KWA MOTO TANGA

Basi kampuni ya Tahmeed lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Mombasa, Kenya limeteketea kwa moto leo Januari 29, mwaka 2018 katika kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni mkoani Tanga. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Handeni, William Nyero amesema polisi wapo eneo la tukio na hakuna madhara yoyote kwa abiria waliokuwa kwenye basi hilo. 

Amesema dereva wa basi hilo baada ya kubaini kasoro aliliegesha pembeni na abiria kuteremka, kushusha mizigo yao.

"Abiria wote waliokuwa wakisafiri na basi hilo wapo salama. Baada ya abiria kushuka na kushusha mizigo yao basi liliwaka moto,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527