ANGALIA PICHA 14 ZA AINA YAKE BARANI AFRIKA WIKI HII

Mvuvi huyu nchini Somalia anaonekana akiwa amembeba papa mkubwa ambaye alimvua baharini. Anaelekea katika soko la samaki la Hamarweyne karibu na mji mkuu wa Mogadishu.

Ijumaa, msichana akitembea karibu na mabaki ya nyumba zilizoharibiwa na maporomo ya ardhi katika mtaa mmoja mjini Kinshasa. Mafuriko huwatatiza sana wakazi wa mitaa ya mji huo mkuu wa DRC kwa sababu nyumba nyingi zimejengwa kwenye maeneo tambarare na mifumo ya kuondoa maji taka ni duni.Siku hiyo pia, mwanamume nchini Sudan anaonekana akiondoka kwenye kiwanda cha kuoka mikate akiwa na mkate mjini Khartoum.Bei ya mkate nchini Sudan imepanda maradufu baada ya serikali kuondoa ruzuku. Polisi wamekuwa wakikabiliana na wanafunzi wanaoandamana kulalamikia kupanda kwa bei.Ijumaa pia, farasi hawa walionekana karibu na magofu ya mji wa Shahhat, Libya uliojengwa na Wagiriki na Warumi.Katika taifa jirani la Algeria, mwanamume anatazama mteremko ulio na theluji katika eneo la Ain Sefra, Algeria katika Jangwa la Sahara Januari 7.Jumatano, mteja jijini Naireobi anaonekana akijaribu kufanya uamuzi wa kiatu atakachonunua miongoni mwa viatu vilivyoundiwa China katika duka moja Januari 10.Na nchini Morocco, mwanamume huyo anaonekana kujawa na upweke akitembea ufukweni wakati wa futani mjini Rabat Jumatatu. Taifa hilo limeshuhudia baridi kali siku za karibuni.Na kasa hawa wadogo wanasubiri kuachiliwa huru katika bahari ya Atlantic nchini Benin... huku mwanaharakati mtetezi wa uhifadhi akionekana akishiriki maonesho ya kuhifadhi kasa Siku ya Taifa ya Kasa eneo la Grand-Popo nchini Benin.Kasa wadogo hufa sana na ni wachache sana hukomaa kufikia ukubwa wa kasa huyu aliyepigwa picha kwenye Bahari ya Sham katika pwani ya Misri siku moja baadaye Papa Tawadros II
Papa Tawadros II, kiongozi wa kanisa la Coptic la Misri, naye anaonekana akiwaongoza waumini kwa ibada mkesha wa Krismasi. Kinyume na Wakristo wengine ambao husherehekea Krismasi mnamo 25 Desemba, kanisa la Coptic husherehekea sikukuu hiyo mnamo tarehe 7 Januari.Kanisa la Kiothodoksi la Ethiopia pia husherehekea Krismasi tarehe 7UJanuari. Hapa, mwumini mmoja anaonekana akisoma Biblia akitumia mshumaa katika mji wa Lalibela kaskazini mwa nchi hiyo.Siku iliyotangulia, waumini wanaaonekana wakitoka nje ya kanisa baada ya kushiriki maoni ya asubuhi katika kanisa la Bete Amanuel, "Nyumba ya Emmanuel".

Picha kwa hisani ya AFP, Reuters na Science Photo Library

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527