WAZAZI MBURAHATI SACCOS YAIVA, KUPATA HATI YA USAJILI HIVI KARIBUNI


Mwenyekiti wa muda wa Wazazi Mburahati Saccos, John Mapunda akifungua mkutano wa wanachama wa Saccos hiyo, uliofanyika kwenye ukumi wa Jengo la Kitegauchumi la CCM, Mburahati, Dar es Salaam, jana. Amesema ameamua yeye na wenzake kuanzisha ushirika huo wa Akiba na mikopo siyo kwa maslahi ya kisiasa bali kuwasaidia kuwasaidia kiuchumi wanachama wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Mburahati ili nao waweze kuwa na maisha bora wakiwa ni miongoni mwa Watanzanaia wenye mahitaji hayo. Kushoto ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo ambaye alifika kwenye mkutano huo kutoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha na kuendesha Saccos. Kulia ni Mhazini wa muda Boniface Chigenda na Katibu wa muda Sofia Kiroboto.
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akitoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha Saccos na kuifanya idumu wakati wa mkutano huo. Amesema Saccos hiyo kwa sasa imeshatimiza masharti yote ya kupatiwa usajili na inapatiwa usajili huo hivi karibuni, alisema katika Kadirio lake Saccos hiyo inatarajia kupata zaidi ya Sh. milioni 13 kutokana na ada na michango ya wanachama ambao hadi sasa wamefikia 68, pia kufanya matumizi ya zaidi ya Sh. milioni 13 na kubaki na ziada ya zaidi ya Sh. milioni 29.
Kitabu au Masharti ya Saccos hiyo
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo, akionyesha orodha ya wananchama 68 waliokwishajiunga na Saccos hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa muda John Mapunda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Mburahati.
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akifafanua jambo wakati akionyesha orodha hiyo 
Baadhi ya wanachama wa Saccos hiyo wakisikiliza Ofisa huyo kwa makini Mwenyekiti wa muda wa Saccos hiyo John Mapunda akitoa nafasi kwa wanachama kuuliza maswali
Mwanachama wa Saccos hiyo Dismas Shirima akiuliza swali.
Mwanachama wa Saccos hiyo Mtindi Mbega akiuliza swali
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo (kushoto), akimsikiliza kwa makini Mwanachama wa Saccos hiyo Justin Kaijage wakati akiulizwa swali
Mwenyekiti wa muda wa Saccos hiyo John Mapunda na Katibu wake Sofia Kiroboto wakifuatilia kwa karibu wakati wanachama wakiuliza maswali
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akijibu maswali
wanachama wakiwa ukumbini
Wanachama ukumbini
Wanachama ukumbini 
Wanachama wakichangamkia kulipa ada 
Wanachama wakichangamkia kulipa ada
Mtoto wa mmoja wa wanachama wa SACCOS akijiburudisha kwa soda wakati mkutano ukiendelea
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo (kulia) akiagana na wanachama waanzilishi wa Saccos hiyo, Dickson Tungaraza, baada ya kikao kumalizika. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527