WAKILI KIBATALA : LULU ANAWEZA KUPATA DHAMANA AKISUBIRI RUFAA KUSIKILIZWA

Wakili wa Elizabeth Michael ‘Lulu’, Peter Kibatala, kufuatia hukumu ya miaka miwili dhidi ya Lulu jana, ametoa ufafanuzi kupitia akaunti yake ya Instagram kuhusu kitakachofuata alipoulizwa maswali na watu wengi ambapo alitumia fursa hiyo kuwafafanulia sheria inavyosema kuhusu nini kinafuata.


Majibu yake kwa maswali hayo ni yafuatayo:

Amesema kuwa hakuna hukumu tofauti inayoweza kutolewa kabla mhukukiwa hajatumikia theluthi ya kufungo chake ambacho kwa Lulu itakuwa ni kuanzia miezi mitano.

Ndani ya hiyo miezi mitano dhamana inaweza kuombwa wakati wakisubiria rufaaa ianze kusikilizwa. Kwa maana hiyo anaweza kutoka kwa dhamana muda wowote mahakama ikmpatia dhamana.

Huwezi kuacha kijana wa miaka 22 mwenye maisha marefu mbele yake ahukumiwe kwa uhalifu kwa sababu ya suala la muda, kwani itaharibu maisha yake ya mbele. Kwa hiyo rufaa imelenga katika kuondoa tatizo hilo.

Kukata rufaaa na kuomba dhamana na kufanya kazi za jamii vinaweza kufanyika kwa wakati mmoja wakati suala hili likisubiriwa kusikilizwa na mahakama ya rufaa.

==>Huu ndo Ujumbe wa Kitabala katika Instagram yake




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527