SERIKALI YAIPONGEZA WCF KWA KUPIGA HATUA KUBWA NDANI YA KIPINDI KIFUPI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Umlemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akifungua mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kwenye ukumnbi wa Simba, Kituo cga Mikutano cha Kimataifa, AICC Arusha leo Novemba 29, 2017

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa mafanikio ambayo Mfuko umeyapata katika kipindi cha muda mfupi tangu uanzishwe.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) jijini Arusha leo Novemba 29, 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema, katika kipindi kifupi cha miaka miwili tangu WCF ianizshwe Mfuko umeweza kutekeleza
wajibu wake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusajili wanachama na kulipa Mafao ya
Fidia.

“Mfuko umeanza kufikia wanyonge kwani umeonyesha
jinsi ambavyo wafanyakazi wanyonge waliokuwa hawalipwa fidia wanapopata madhara kazini, sasa kutokana na kuwepo kwa Mfuko huu wanyonge wameanza
kufaidi matunda kama ambavyo serikali ilidhamiria.

“Nitoe wito kwa viongozi wa Mfuko, endeleeni
kutoa elimu kwa wananchi hususan waajiri ili waweze kujisajili na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuwalipa fidia wafanyakazi wao pindi wanapopata madhara wawapo kazini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw.
Masha Mshomba amesema hali ya Mfuko ni njema tangu uanzishwe, “Tunapokutana leo hii kwa mara ya
kwanza kabisa, napenda kuwajulisha kuwa Mfuko umekuwa ukifanya vizuri katika kuimarika kifedha ambapo kwa mwaka wa kwanza tu, Mfuko ulifikia kiasi cha shilingi Bilioni 65.68 na katika mwaka wake wa pili ambapo ndiyo huu tulio nao napenda kuwafahamisha kuwa Mfuko umekuwa hadi kufikia Shilingi Bilioni 135 fedha ambazo bado hazijakaguliwa lakini sitarajii tofauti kubwa sana hata zoezi la ukaguzi litakapofanyika”,amesema Bw. Mshomba.

Aidha Bw. Mshomba alisema, madhumuni ya Mkutano huu wa siku mbili ambao umebeba kauli mbiu ya "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”. ni kutoa taarifa ya mwaka ya Mfuko, kutathmini maendeleo na changamoto zinazoukabili Mfuko na kupokea maoni ya kuboresha huduma za Mfuko.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini
ya WCF, Bw. Emmanuel Humba amesema, tangu Mfuko uanzishwe, umetoa mafunzo mbalimbali kwa wadau wa Mfuko ikiwa ni pamoja na Madaktari.

“Hadi sasa Mfuko umetoa mafunzo kwa Madaktari
504 nchi nzima kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini za ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi”, amesema Bw. Humba.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Anthony Mavunde, akitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mashomba, akitoa hotuba yake 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, wakati alipowasili kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha leo Novemba 29, 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakati akiwasili kqwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC jijini Arusha
Mhe. Mhagama na viongozi wengine wakiimba wimbo wa taifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, akipokelewa na  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar
Mbunge wa Chalinze, Mhe., Ridhiwani Kikwete, (kulia), akizungumza na Mkurugenzi wa Operesheni wa WCF, Bw. Anslem Peter.
Afisa wa WCF, Bw. Edward Kirenga, (kushoto), akiwasajili wajumbe wa mkutano
Kutoka kushoto, Mhe. Waziri Mhagama, Dkt. Irine Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akitoa hotuba yake.

Dkt. Isaka, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Stella Ikupa, (kushoto), wakati wa mkutano huo.
Kikundi cha bendi ya Mjomba, (Mrisho Mpoto), kikitumbuiza
Viongozi wakishuhudia burudani ya kikundi cha bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto.
Mkurugenzi wa Operesheni wa WCF, Bw.Anselim Peter, (wa pili kulia), akijadiliana jambo na maafisa wa Mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Dkt. Irine Isaka, (kulia), akisalimiana na Meneja Mafao wa WCF, Bi. Rehema Kabongo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA), Meshac Bandawe , (kushoto), akisalim iana na Meneje Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele
Wajumbe wamkiendelea kusajiliwa kabla ya kuingia ukumbini.
Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Emmnuel Humba, (kulia), akibadilishana mawazo na wajumbe wenzake wa bodi, Dkt. Francis Michael, (wa pili kulia), na Bw.Richard Wambali
Baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa WCF 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527