ROBERT MUGABE AONEKANA HADHARANI...ANAYEMRITHI BADO HAJAJULIKANA

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.

Alihudhuria sherehe za kufuzu kwenye mji mkuu Harare.

Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.

Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumzo hayo haraka iwezekanavyo.

Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.

Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kumfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua uongozi wa Zanu-PF na urais.

Chanzo-BBC
Theme images by rion819. Powered by Blogger.