PATCHO MWAMBA : LULU HAKUMUUA KANUMBA BALI ALIKUWA SHAHIDI WAKATI ANAKUFA

Mwanamuziki na Muigizaji nchini, Patcho Mwamba ameifungukia kauli ya Mama Kanumba ya kushukuru kitendo cha Muigizaji Lulu kufungwa miaka miwili kwa kosa la kumuua bila kukusudia muigizaji Kanumba na kusema kwamba hakuna haja ya kuendelea na 'beef' kwani hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba hai.


Patcho ambaye alikuwa muigizaji na rafiki wa karibu na Marehemu Steven Kanumba amesema kwamba Mama kanumba anapaswa kuwa na moyo wa kusamehe kwa sababu binti huyo akimaliza kifungo atarudi mtaani na ataendelea na maisha yake hivyo kujengeana chuki siyo jambo jema.


"Sina la kusema juu ya jukumu ya Lulu, lakini Mahakama imeamua kama ilivyoamua, kwa upande mmoja kuna unafuu kwani kwa kesi ile kufungwa miaka miwili ni bahati, ukija upande wa pili inaumiza sana kwani jela siyo sehemu nzuri sana kwa mtu kuwepo kila mtu anajua hilo hasa ukizingatia bado ni mdogo hivyo tumuombee Mungu ampe nguvu, uwezo naamsaidie aweze kustahimili hiyo hali" Patcho.


Aidha Patcho ameongeza "Nimemuona mama anasema anashukuru (Mama Kanumba) haki imetendeka, mimi sidhani kama kunahitajika kuwepo na ma Beef. Mwanaye, ambaye pia ni rafiki yetu ameondoka lakini tunaamini ni mipango ya Mungu. Hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba aishi. kusema naenda kumzika Kanumba upya sidhani kama kuna haja ya kuendeleza ma beef japo yapo. End of the day Lulu atatoka wataongea vizuri?. Sidhani yule mama yangu hivyo simshauri aendee kuwa na kinyongo".


Patcho amemalizia na kusema kwamba "Kusema kufungwa kwa Lulu kutampatia unafuu sidhani ni uongo yeye aendelee kuwa mama maana ninachoamini Lulu hakumuua Kanumba bali alikuwa shahidi wakati Kanumba anakufa ndichi ninachokiamini. Baadaye Lulu atatoka jela je ukimuon utamgonga na gari? au Mama Lulu utaweza kuongea naye na wale ni Wahaya ni kabila moja. Sidhani kama Lulu alikuwa akikaa na kufikiria ipo siku atamuua Kanumba".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527