NYALANDU AVAA RASMI GWANDA LA CHADEMA...ASEMA SAA YA MABADILIKO IMEFIKA...

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana amemkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, Jijini Mwanza katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu kwenye kampeni ya kumnadi mgombea udiwani Godfrey Mahame.

"Nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya kupigania mageuzi ya kisiasa na ya kiuchumi Tanzania," amesema Nyalandu baada ya kukabidhiwa kadi.

Amesema ana shauku, furaha na heshima kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa Chadema. Nyalandu ameongeza kuwa katika majira na nyakati ambazo Taifa linapitia, mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania ni lazima.

"Naungana na chama hiki pendwa ili tutembee pamoja mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji tuwaambie wananchi wakati wa ukombozi ni sasa," alisema Nyalandu.

"Saa ya mabadiliko imefika kwa mtu yeyote miongoni mwetu, tumepewa utayari wa kubadilisha mwelekeo wa nchi," amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527