MKE WA LAZARO NYALANDU,FARAJA KOTA AVUNJA UKIMYA

Faraja Kota ambaye ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza jinsi alivyojawa na hofu baada ya mfululizo wa matukio ya wiki nzima tangu mumewe atangaze kujiondoa ndani ya CCM.

Mwanamke huyo aliyewahi kutwaa taji la Miss Tanzania katika mtandao huo ameandika “If only you knew how terrified I am.” Akimaanisha laiti ungejua ni kiasi gani nimejawa hofu.

Hata hivyo, wafuasi wake katika mtandao huo katika maoni yao wamemtoa hofu huku naye akiwajibu kuashiria kukubaliana nao na jinsi wanavyomuunga mkono katika kipindi hiki.

Mmoja wa wafuasi wake Becky Bavuna ameandika majeshi yaliyo upande wenu ni mengi kuliko haya ya dunia naye Faraja amemjibu akisema: “Amen”.

Mwingine amemwandikia ujumbe akisema: Mungu awatie nguvu muyaweze yote katika yeye awatiaye nguvu. You will be in my prayers”. Naye Faraja akajibu tafadhali endelea kutuombea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527