MIKOA YOTE TANZANIA YAAGIZWA KUPIMA WANANCHI VIRUSI VYA UKIMWI (HIV)


MIKOA yote nchini imeagizwa kuwapima wananchi wake, virusi vya ukimwi (HIV) bure kwenye wiki ya kuadhimisha Siku ya Ukimwi.


Wiki hiyo inaanza Novemba 24 na kuisha siku ya kilele cha Siku ya Ukimwi duniani Desemba Mosi. Kaulimbiu ni “Changia mfuko, okoa maisha, Tanzania bila Ukimwi inawezekana”. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema hayo jana.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika kitaifa Dar es Salaam. Aliagiza kupatikana wataalamu wa kutosha kwa kila mkoa kwa upimaji huo na ushauri nasaha.

Alisema katika wiki hiyo, kutazinduliwa Ripoti ya utafiti wa kitaifa wa virusi vya Ukimwi, utafiti ambao hufanyika kila miaka minne. Alitaja shughuli nyingine ni uzinduzi wa mkakati wa kondom wa kitaifa, kongamano la kitaifa la wataalamu watakaojadiliana kukabili Ukimwi na huduma ya kupima kwa hiari.
Chanzo-Habarileo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527