KAMATI YA MAADILI YA BUNGE YAMHOJI SAED KUBENEA KUDHARAU BUNGE

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.


Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.

Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika jana baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokuwa katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe.

Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi.

“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.