JENGO LA CLOUDS MEDIA LAUNGUA MOTO


Habari kutoka jijini Dar es salaam zinasema kuwa sehemu ya jengo la Clouds Media limeungua moto.

Moto huo umezuka katika ofisi za Clouds Media Group na kusababisha Television na Radio Clouds kutokuwa hewani kwa muda.

Moto huo ulianza saa 4 asubuhi leo Jumanne Novemba 21,2017 katika chumba kimoja kwenye ghorofa ya kwanza uliosambaa kwenye jengo la kampuni hiyo.

Taarifa za awali zinasema moto huo umetokana na hitilafu ya umeme kwenye chumba cha kurushia matangazo cha Clouds TV.
Magari ya Zimamoto yapatayo manne yalifika eneo la tukio kwa ajili ya kuzima moto huo.

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds, Ruge Mutahaba amesema amewashukuru Zimamoto kwa kuweza kuokoa vifaa na kuzima moto huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527