Balaa!! MWANAUME AKUTA MAMBA MKUBWA NJE YA NYUMBA YAKE

Mwanamume mmoja katika kijiji kilicho jimbo la mashariki mwa India la Orissa, alipigwa na mshangao baada ya kumpata mgeni ambaye hakumtarajia nje ya nyumba yake - mamba wa urefu wa mita 3

Dasharath Madkami alimpata mamba huyo baada ya kuamshwa na sauti zisizo za kawaida usiku.

Alipiga kamsa na wanavijiji wakafika ambao walimfunga mamba huyo kwa mti.

Mamlaka za wanyamapori kisha zikafika kumuokoa mnyama huyo.

Hata hivyo kulikuwa na mzozo kuhusu ni wapi mambaohuyo angepelekwa.


Maafisa wa misitu walitaka kumuachilia myama huyo kwenda kwa bwagwa lililoku karibu ambapo alitoka, lakini wanavijiji wakakataa wakohofia kuwa angerudi tena.

Mamba huyo hata hivyo aliachiliwa kwenda mto Balimela ulio umbali wa kilomita 60.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527