Angalia Picha : UZINDUZI MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI MKOA WA SHINYANGA MWAKA 2017


Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Novemba 13,2017 umezindua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yenye kauli mbiu "Zuia ajali,Tii sheria,Okoa Maisha". 



Uzinduzi huo umefanyika katika Viwanja vya Zimamoto mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack. 


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani,Matiro aliwataka wasimamizi wa sheria za usalama barabarani kuwa wakali kwa wasiotii sheria za barabarani na kuhakikisha wanawafikisha mahakamani pamoja na kuwanyang’anya leseni zao. 

“Tusiwafumbie macho wanaovunja sheria na kugharimu maisha ya wananchi,hakikisheni kuwa vyombo vyote vya usafiri vinavyoingia barabarani vinafuata masharti na vigezo vinayotakiwa na wahusika”,alisema. 

Aidha aliwataka baadhi ya askari wasiokuwa waaminifu kwa kuendekeza rushwa na kupindisha kesi za watu wanaovunja sheria kuacha tabia hiyo mara moja.

 Katika hatua nyingine alilitaka jeshi la polisi kutoa elimu kuhusu masuala ya usalama barabarani katika shule za msingi na sekondari ili wanafunzi wajue matumizi sahihi ya barabara.

Matiro aliwakumbusha akina mama wanaopanda katika pikipiki na baiskeli kuacha tabia ya kukaa upande bali wakae mkao wa ‘kiume’ ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima. 

Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule alisema lengo la maadhimisho hayo ni kutafakari na kukumbushana mambo mbalimbali ya usalama barabarani yakiwemo ya uzingatiaji wa taratibu,kanuni na sheria za barabarani ili kujiepusha na ajali hivyo kuwataka watumiaji wa barabara kuzuia ajali kwa kutii sheria za barabarani ili kuokoa maisha. 

Awali akitoa taarifa ya usalama barabarani,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Masanzu alisema kupitia wiki ya nenda kwa usalama wananchi watumiaji wa barabara watanufaika kwa kupata elimu kwani kuna mabanda mbalimbali ya usalama barabarani. 

Masanzu alisema mkoa wa Shinyanga bado una changamoto ya ajali za barabarani zinazosababisha vifo,ulemavu na umaskini huku sababu ikiwa ni makosa ya kibinadamu,ubovu vya vyombo vya barabarani na mazingira ya barabara. 

“Chanzo kikubwa cha ajali ni makosa ya kibinadamu kama vile mwendokasi,kulipita gari lililo mbele bila kuchukua tahadhari,kutoheshimu alama na michoro barabarani,abiria kushabikia mwendokasi,kuzidisha abiria na mizigo,ulevi,kutovaa kofia ngumu na kutokuwa na elimua usalama barabarani”,alieleza. 

Hata hivyo Masanzu alisema takwimu za ajali mkoani Shinyanga zinaendelea kupungua ambapo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba 2016 kulikuwa na ajali 169 na kuanzia mwezi Januari hadi Septemba 2017 ajali zilizotokea ni 144 sawa na upungufu wa ajali 25 sawa na asilimia 8. 

Alisema jeshi la polisi limeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na ajali ikiwemo matumizi ya speed radar (kamera za tochi),kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara,kufanya doria kwenye barabara kuu na kushirikiana na wadau wote wa usalama barabarani. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji alisema asilimia 80 ya ajali zinazotokea mkoani humo zinasababishwa na makosa ya kibinadamu huku akiongeza kuwa ajali nyingi ni za pikipiki na baiskeli.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizindua wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga kwa  niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack leo Jumatatu Novemba 13,2017 katika viwanja vya Zimamoto mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kwa  niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Masanzu  akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga
Wananchi wakiwa katika eneo la tukio
Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiswali wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani
Viongozi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa meza kuu
Meza kuu wakiwa wamesimama kupokea maandamano ya askari wa kitengo cha usalama barabarani,wanafunzi na watumiaji wa barabara
Maandamano yakiingia katika viwanja vya Zimamoto mjini Shinyanga 
Waandamanaji wakipita mbele ya mgeni rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Wanafunzi wakiandamana
Waendesha bodaboda na bajaji wakiwa katika maandamano
Kwaya ya AIC Kambarage ikitoa burudani
Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
MCT Band ikitoa burudani

ZAMU YA KUTEMBELEA MABANDA IKAWADIA
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa katika banda la jeshi la polisi akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa kikosi cha usalama barabarani kuhusu kifaa kinachotumika kupima kilevi kwa madereva wa vyombo vya moto
Afisa wa kikosi cha usalama barabarani akionesha kifaa cha kubaini mwendokasi "Speed radar" maarufu kamera ya tochi
Afisa wa kikosi cha usalama barabarani akionesha picha mbalimbali za makosa yanayofanyika barabarani
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akipokelewa katika banda la Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SHUWASA)
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika banda la VETA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika banda la benki ya NMB
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika banda la TTCL
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifurahia jambo katika banda la benki ya Posta 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika banda la TANROADS
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akiendelea kutembelea mabanda
Maafisa wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa na wadau
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa na na maafisa wa jeshi la polisi na wadau wa masuala ya usalama barabarani.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527