AMUUA MKEWE BAADA YA KUKATAA KUSHIRIKI NAYE TENDO LA NDOA

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamume mmoja katika jimbo la kaskazini mwa India la Haryana amemuua mkewe baada ya kukataa kushiriki naye tendo la ndoa.

Sanjiv Kumar mwenye umri wa miaka 35 alidaiwa kumyonga mkewe ,Suman wakati wa vita siku ya Jumanne.

Mwanamume huyo alikiri kutekeleza kitendo hicho baada ya kukamatwa , afisa wa polisi Ramesh Jaglan aliambia BBC.

Migogoro ya kinyumba ndiyo yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

''Alikuwa akikataa kufanya ngono kwa muda .Siku ya Jumanne alikataa tena, hatua iliyomuudhi na kuamua kumnyonga.Tumemkamata'', bwana Jaglan aliambia BBC.

Wanandoa hao walikuwa wameoana kwa zaidi ya muongo mmoja. Wana watoto wawili.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527