WAAJIRI WA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI JIJINI MWANZA WALAUMIWA


Mkufunzi wa mafunzo kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani katika Kata ya Buhingwa Jijini Mwanza, akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo hii leo. Mafunzo hayo yafanyika kwenye ukumbi kwa kanisa la AICT Buhingwa kuanzia jana na yatafikia tamati kesho Oktoba 12,2017. Na George Binagi-GB Pazzo
****

Baadhi ya waajiri wa watoto wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wameelezwa kuwa kikwazo cha kuwaruhusu watoto hao kupata elimu ya utambuzi yanayotolewa na shirika la WoteSawa.

Mratibu wa shirika hilo linalotetea haki na maslahi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani, Cecilia Nyangasi ameyasema hayo hii leo wakati wa mafunzo kwa watoto wafanyakazi katika Kata ya Buhongwa jijini Mwanza.

“Waajiri wamekuwa ni changamoto kubwa kwa sababu wengi wao wanadhani kwamba tunakuja kuwapotosha watoto wao”. Alisema Nyangasi na kubainisha kwamba shirika la WoteSawa linatoa
elimu ya kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao kisheria, wajibu wao kazini pamoja na elimu ya afya ya uzazi ili kuondokana na mimba za utotoni.


Nyangasi alisema baada ya mafunzo hayo ya siku tatu kuanzia jana, itaundwa kamati ya watoto wafanyakazi wa nyumbani Kata ya Buhongwa kama ilivyofanyika kwenye Kata za Nyakato, Mecco, Isamilo, Pasiansi, Kirumba na Mkuyuni ambapo jukumu kubwa la
kamati hizo ni kuwa mabalozi wa watoto wengine ambao hawakufikiwa na mafunzo
hayo.

Suzana John na Lugwisha Zakaria ambao ni baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyojumuisha watoto 47 katika Kata hiyo ya Buhongwa, wamesema mafunzo hayo yamewasaidia
kutambua haki zao kisheria na pia wajibu wao kama waajiriwa.

Mwanasheria Joseph ambaye ni mkufunzi wa mafunzo hayo
Mkufunzi wa mafunzo hayo akifafanua jambo
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoanza jana katika Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza akiuliza swali
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoanza jana katika Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza akiuliza swali
Washiriki wa mafunzo hayo katika Kanda ya Buhongwa Jijini Mwanza
Washiriki wa mafunzo hayo katika Kanda ya Buhongwa Jijini Mwanza
Mratibu wa WoteSawa, Cecilia Nyangasi (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo
Afisa kutoka shirika la WoteSawa la Jijini Mwanza
Suzana John, mshiriki wa mafunzo hayo
Lugisha Zakari, mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.

Bonyeza HAPA kusoma zaidi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments