RAIS MAGUFULI AGOMA KUFUTA MWENGE WA UHURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema hatafuta Mwenge wa Uhuru katika kipindi chake cha uongozi kwa sababu una faida mbalimbali kwa taifa.


Hayo ameyasema leo kwenye hotuba yake wakati akihitimisha mbio za Mwenge mwaka huu sambamba na kuazimisha miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.


Rais Magufuli amesema kwenye awamu yake kamwe hatafuta mbio hizo kwani zina saidia kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na kumuenzi Baba wa taifa Hayati Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa Mwenge wa Uhuru.


“Nafahamu kuna watu wanataka mbio za Mwenge zifutwe kwa kisingizio cha gharama lakini wanasahau kuwa Mwenge huo unasaidia kuanzishwa na kukamilika kwa Miradi ya maendeleo nchini. Nataka niwahakikishie kuwa kwenye uongozi wangu na Dkt. Shein hatutafuta Mwenge wa Uhuru”, amesema Rais Magufuli.


Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa mbio za Mwenge zimekuwa zikisaidia kubaini madudu mbalimbali yanayofanyika kwenye Halmashauri nchini ikiwemo Miradi hewa. Rais ameahidi kuipitia ripoti nzima ya mbio hizo na kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyoainishwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments