POLISI WAUA WATUHUMIWA WALIOMJERUHI MEJA JENERALI MSTAAFU

KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI NA KUPATIKANA KWA SILAHA AINA YA SMG RISASI KUMI NA TISA NA MAGANDA MAWILI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 11.10.2017 majira ya saa nne kamili usiku huko maeneo ya Mbezi Mshikamano kwa Mgalula, askari walipata taarifa kutoka kwa FRANCIS MINDE miaka 30, mfanyabiashara ambaye anamiliki duka la vitu mchanganyiko kwamba walifika watu wawili katika duka lake wakitumia pikipiki aina ya Boxer nyeusi ambayo haikusomeka namba na kumuuliza kama kuna huduma ya M-PESA na TIGO-PESA na kuwajibu kuwa hakuna huduma hiyo, aliwatilia mashaka huenda sio watu wazuri hatimaye alitoa taarifa Polisi.

Mara baada ya kupata taarifa hizo askari walikwenda eneo hilo na kuiona pikipiki ikiwa imeegeshwa gizani ikiwa na watu watatu, askari waliwaita watu hao ili kuwahoji lakini watu hao walianza kukimbia huku wakifyatua risasi upande waliopo askari, kuona hivyo askari nao walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi wawili, mmoja kati yao alifanikiwa kukimbia na pikipiki waliyokuwa nayo

Aidha eneo la tukio ilikutwa Silaha aina ya SMG yenye namba UC59821998 ikiwa na magazine mbili, magazine moja ikiwa na risasi kumi na tisa (19) na nyingine ikiwa tupu na maganda kumi na tatu (13) ya risasi aina ya SMG.

Katika ufuatiliaji wa tukio hilo ilibainika kuwa mmoja wa majambazi hao waliouwawa ni miongoni mwa watuhumiwa walioshiriki tukio la kuvamiwa kwa Meja Generali mstaafu wa Jeshi la Wananchi VICENT KARIONGO lililotokea mnamo tarehe 11/09/2017 majira ya saa kumi na moja jioni.

Majeruhi wote wawili walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala. Hakuna askari aliyeumia au kujeruhiwa, miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala. Jitihada za kumtafuta jambazi aliyekimbia zinaendelea.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 12.10.2017 majira ya saa nane na nusu usiku huko maeneo ya Mbezi Luis, Tegeta “A” askari walipata taarifa kuwa katika Bar iitwayo TUMAINI, kuna majambazi ambao idadi yao haijajulikana wakiwa na gari no. T 563 TAH aina ya Toyota Noah rangi ya Blue ikiwa imetolewa viti vyote vya nyuma na kubaki siti ya dereva na abiria, lengo lao lilikiwa ni kupakia vitu ambavyo wangeiba kwenye Bar hiyo.

Wakati wakiendelea na uvunjaji askari walifika eneo la tukio na baada ya kugundua askari wamefika majambazi hao walifanikiwa kukimbia na kutelekeza gari hilo, majambazi hao hawakufanikiwa kuchukua mali yeyote na gari lipo kituo cha Polisi. Ufuatiliaji unaendelea wa kujua mmiliki wa gari lililotumika katika tukio hilo.

POLISI KANDA MAALUM DSM KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUANZIA TAREHE 06.10.2017 HADI TAREHE 11.10.2017 KIMEFANIKIWA KUKUSANYA TSH 466,350,000/= KWA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam kupitia Kikosi chake cha Usalama barabarani kinaendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 06.10.2017 hadi tarehe 11.10.2017 kama ifuatavyo:-
  1. Idadi ya magari yaliyokamatwa – 14,340
  2.     Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa – 413
  3.     Daladala zilizokamatwa -5,024
  4.     Magari mengine (binafsi na malori) -1,205
  5.     Bodaboda waliofikishwa Mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmet na kupakia mishikaki -15
  6.     Jumla ya Makosa yaliyokamatwa – 15,545
  7.     Fedha za Tozo zilizopatikana – 466,350,000 /=
  8.     Magari yaliyokamatwa kutokana na Kuchelewa kulipa faini kwa wakati – 2,832 (zaidi ya siku 7)

    Kiasi kilicholipwa – 264, 673,4000/=

L .B.MAMBOSASA – SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments