Picha : DC SHINYANGA AKABIDHI SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili katika manispaa ya Shinyanga.

Zoezi la kukabidhi sare hizo za shule limefanyika leo Alhamis Oktoba 12,2017 katika shule ya msingi Kitangiri.

Msaada huo wa sare za shule unatokana na kampeni iliyoanzishwa na mkuu huyo wa wilaya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi sare hizo,Matiro alisema pamoja na serikali kuwa na sera ya elimu bure lakini wamebaini kuwa kuna watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu hivyo wanahitaji msaada kutoka wadau mbalimbali.

“Tulifanya zoezi la kugawa sare kwa wanafunzi wengine hivi karibuni,na leo ofisi yangu kwa kushirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO) nimekuja kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 121 wa kata ya Kitangili na Kizumbi”,alieleza Matiro.

Matiro aliwataka wazazi kutimiza wajibu wao wa kulea watoto badala ya kuwatekeleza kwa bibi na babu zao na wao kukimbilia mjini huku watoto wakiteseka na kuishi katika maisha magumu.

Kwa upande wake Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny Raymond alisema walifanya utafiti na kubaini kuwa kuna wanafunzi/watoto wengi katika kata ya Kitangili na Kizumbi wanaishi katika mazingira magumu hivyo kushirikiana na wadau wengine kutafuta sare za shule kwa ajili ya wanafunzi hao.

“Tumebaini kuwa watoto wengi hawaishi na wazazi wao,wengine ni yatima,lakini pia wapo ambao wazazi wao hawana uwezo kiuchumi hali inayosababisha watoto kushindwa hata kuhudhuria masomo yao,wakitumika kama chanzo cha mapato katika familia zao”,alisema Raymond.

Naye Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim mbali na kushukuru kwa msaada huo wa sare za shule zikiwemo kaptura,sketi na mashati na kueleza kuwa kutokana na ugumu wa maisha wapo watoto wanashindwa kupata chakula na wengine kukosa mavazi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza kabla ya kuanza kugawa sare za shule kwa wanafunzi 121 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kizumbi na Kitangili leo katika shule ya msingi Kitangili mjini Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro  akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akiwataka akina mama kuunda vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujiinua kiuchumi
Mratibu wa miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO),Venny Raymond akielezea namna walivyowapata watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata ya Kitangili na Kizumbi
Afisa Elimu kata ya Kitangili Mahmood Ibrahim akizungumza wakati wa zoezi la kugawa sare hizo za shule
Diwani wa viti Maalum kata ya Kitangili Mariam Nyangaka (CCM) akimshukuru mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kushirikiana na wadau kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wazazi,walezi na wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kabla ya kugawa sare  za shule kwa wanafunzi hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akimvalisha shati mmoja wa wanafunzi hao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akishikana mkono na mwanafunzi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akivalisha sare ya shule mwanafunzi
Mwanafunzi akiwa ameshikilia sketi baada ya kuvalishwa shati na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akitafakari jambo wakati wa kugawa sare za shule
Zoezi la kugawa sare za shule likiendelea.Wa kwanza kushoto ni Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Miradi kutoka shirika linalohusika na wanawake na watoto la Promising World For Women and Children Organization (PWWCO).
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizumbi Marcelina Bwathondi akijiandaa kumpa sare ya shule mmoja wa wanafunzi hao
Wazazi na walezi wa wanafunzi wakishuhudia zoezi la ugawaji sare za shule kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments