Picha: ASKOFU MKUU WA KANISA LA AICT SILASI KEZAKUBI AFUNGUA PASTORETI MPYA YA KANISA LA AICT MTO JORDAN KAHAMA MJINI


Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi leo Jumapili Oktoba 15,2017 amezindua na kufungua Pastoreti mpya ya Kanisa la AICT Mto Yodani lililopo Shunu mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Ibada ya uzinduzi na ufunguzi wa kanisa hilo imehudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga,ambapo askofu Kezakubi pia alihubiri katika Ibada ya Jumapili katika kanisa hilo.

Akizungumza kanisani hapo,Askofu Kezakubi aliwataka viongozi na waumini wa kanisa hilo kutumia jengo hilo kwa ajili a ibada na siyo vinginevyo.

“Nimefungua kanisa hili mlitumie kwa ajili ibada,pia kuwaita watu wengine waje kusikia neno la mungu ,sitaki kusikia mnatumia nyumba hii ya ibada kutukanana na kufanya mambo yasiyompendeza Mungu”,alieleza Askofu Kezakubi.

“Ni aibu kusikia kelele kwenye kanisa,watu kutukanana kwene nyumba ya Mungu,kama kuna mabaraza yanafanyika kanisani basi yafanyike kama ibada,vivyo hivyo upande wa kwaya,sitaki kusikia mtu anatukuzwa kanisani,mwenye kutukuzwa ni Mungu pekee”,aliongeza Askofu Kezakubi.


Katika hatua nyingine alisema mchungaji ndiye mwalimu na msimamizi mkuu wa masuala ya kiroho hivyo kuwataka wachungaji kufanya kazi yao vyema kwa kuepuka kuwa wavivu na kutolegea kuwaombea na kuwatembelea waumini.

Askofu Kezakubi alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha baadhi ya watu wanaopinga viongozi wa dini  kwenye makanisa kuacha tabia hiyo kwani wanakwamisha kazi ya Mungu huku akiwataka viongozi na waumini kushikamana katika kumtumikia Mungu.

"Kuna watu wapo kwenye makanisa yetu kwa bahati mbaya,wakiingia kanisani wanaanza vita badala ya kuwaunga mkono viongozi wao ili wafanye kazi yao vizuri,wakristo mnatakiwa pia kuwatunza watumishi wa mungu,tuwatunze watu waliolitumikia kanisa kwani tusipowatunza tunakosa baraka",alieleza Askofu Kezakubi.

Aidha aliwataka viongozi wa kanisa hilo kuiombea serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo viovu.

"Wakristo mnapaswa kumtii mungu,tuenende katika maisha anayotaka bwana,tusimame imara na kukataa mambo mabaya,kama mtu ataliharibu hekalu la Mungu,Mungu atamharibu mtu huyo",alisema.

Akisoma risala Mwalimu Lucas Matanya alisema Kanisa la AICT Mto Jordani lilianzishwa Novemba 13,2013 chini ya Mwinjilisti Nicodemus Lufega likiwa na wakristo 7 wakisali chini ya mti na baadae idadi iliongezeka kidogo wakajenga banda ambapo waliendelea na ibada katika eneo la Lugela mtaa wa Shunu mjini Kahama.

“Kanisa hili limekuwa tawi la AICT Kahama Mjini na kwa ushirikiano uliopo,walinunua eneo na kuanza kujenga jengo hili la kuabudia na nyumba ya kichungaji,choo na kuweka uzio,lengo likiwa ni kuhakikisha wanapata huduma za kiroho karibu na makazi yao”,alieleza.

Aidha alisema Baraza la Utumaji la Dayosisi ya Shinyanga limemtuma Mchungaji Daudi Kazimoto kuwa mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan.

Alizitaja changamoto zinazolikabili kanisa hilo kuwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kununulia eneo ili kupanua eneo la kanisa kwani lililopo ni dogo lakini pia ukosefu wa jengo la utawala.

Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio wakati uzinduzi wa kanisa hilo na ibada ya Jumapili

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akizungumza kabla ya kuzindua kanisa la AICT Mto Jordan leo Jumapili Oktoba 15,2016 mjini Kahama-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waumini wa kanisa la AICT Mto Jordan wakishuhudia zoezi la ufunguzi wa kanisa hilo

Mchungaji Elias Buluba kutoka kanisa la AICT Kahama Mjini akisoma neno la Mungu wakati wa zoezi la kuzindua kanisa la AICT Mto Jordan

Mwalimu Lucas Matanya akisoma risala kuhusu kanisa hilo jipya
Waumini wa kanisa hilo wakishuhudia zoezi la uzinduzi wa kanisa hilo
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi  akizungumza wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi  akikata utepe
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akisoma maandishi baada ya kukata utepe


Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akifungua kufuli ili aingie kwenye kanisa jipya la AICT Mto Jordan
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiingia kanisani
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiingia kanisani

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiwapungia mkono waumini wa kanisa la AICT walioingia katika kanisa la AICT Mto Jordan
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza ibada fupi ya ufunguzi wa kanisa la AICT Mto Jordan
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza ibada katika kanisa la AICT Mto Jordan

Waumini wa kanisa la AICT wakiwa kanisani

Mchungaji Elias Buluba kutoka kanisa la AICT Kahama Mjini akizungumza wakati wa ibada hiyo
Viongozi mbalimbali wakiwa kanisani
Muonekano wa kanisa la AICT Mto Jordan 
Muonekano wa kanisa la AICT Mto Jordan

Kiongozi wa Ibada ya Jumapili leo Oktoba 15,2017,Mchungaji Adam Nzoka akizungumza baada ya uzinduzi wa kanisa la AICT Mto Jordan
Mchungaji Elias Buluba kutoka kanisa la AICT Kahama Mjini akizungumza wakati wa ibada katika kanisa la AICT Mto Jordan baada ya uzinduzi wa kanisa la AICT Mto Jordan

Waumini wa kanisa hilo wakifuatilia ibada
Viongozi wa kanisa la AICT wakisali wakati wa ibada ya Jumapili. Kulia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan,mchungaji Daudi Kazimoto,katikati ni Makamu wa Askofu kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Aron Malyuta na kushoto ni Mchungaji Adam Nzoka

Kaimu Katibu Mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga ,Mchungaji Timoth Shadrack akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria zoezi la uzinduzi wa kanisa la AICT Mto Jordan

Mchungaji Simon Temu kutoka kanisa la AICT Ngudu mkoani Mwanza akijitambulisha

Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aron Malyuta akitoa neno wakati ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Mto Jordan



Viongozi wa kanisa la AICT wakiwa wamesimama kabla ya Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi hajaaza kuhubiri neno la Mungu katika kanisa la AICT Mto Jordan

Kikundi cha sifa wakiimba wimbo wa kuabudu

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi ambaye ndiye Mlezi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga akitoa mahubiri wakati wa Ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Mto Jordan baada kuzindua kanisa hilo

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiendelea na mahubiri

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akimtambulisha 
Mchungaji Daudi Kazimoto kuwa ndiye mchungaji kiongozi wa kanisa la AICT Mto Jordan.

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akieleza sifa za Mchungaji Daudi Kazimoto ambaye amebobea katika neno la Mungu hivyo ana uweza mkubwa wa kuongoza hilo na kuwataka waumini wa kanisa hilo kumpa ushirikiano

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza zoezi la mchango kwa ajili kupanua eneo la kanisa la AICT Mto Yordan

Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Silasi Kezakubi akiongoza zoezi la changizo hilo
Kwaya kutoka AICT Kahama Mjini wakimwimbia Mungu

Viongozi wa Kanisa la AICT wakiwa katika Ibada ya Jumapili

Viongozi wa kanisa la AICT wakiwa katika ibada ya Jumapili

Waimbaji kutoka kwaya ya AICT Kahama Mjini wakiimba na kucheza

Waumini wa kanisa la AICT wakiwa katika ibada ya Jumapili

Emmaus  Gospel Band wakiimba na kucheza

Emmaus  Gospel Band wakiendelea kucheza na kuimba

Viongozi mbalimbali wa kanisa la AICT wakiwa katika ibada ya Jumapili

Kwaya ya Akina Mama wakiimba wakati wa ibada hiyo

Ibada inaendelea

Kwaya ya AICT Bethelehemu mjini Kahama wakiimba na kucheza









Kwaya ya AICT Majengo wakiimba na kucheza

Kwaya ya AICT Galilaya Mhongolo ikiimba

Kwaya ya AICT Nyakato ikiimba

Kwaya ya Waberoya wakiimba

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments