IHEMBE MABINGWA KOMBE LA MBUNGE WA KARAGWE


Mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimpokea mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba
Mgeni rasmi akiwasili katika uwanja wa changarawe ilipofanyika fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akikagua vikosi vya Ihembe na Nyaishozi
Mchezaji wa Ihembe akipiga mpira wa kona
Uwanja wa Changarawe ulihosheheni mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu
Ihembe wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza
Wadau wakishuhudia mtanange toka jukwaa la “mzunguko”
Wachezaji wa Ihembe wakiwa wamemzunguka golikipa wao baada ya kupata kash kash
Mashabiki wa Nyaishozi wakifuatilia kwa makini mchezo wa Bashungwa Karagawe Cup
Kombe likikabidhiwa kwa mgeni rasmi
Mbunge wa Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akitoa neno la pongezi kwa timu zote shiriki 
Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime akimkabidhi kombe nahodha wa Ihembe 
Ihembe wakifurahia kombe lao la ubingwa wa Bashungwa Karagwe Cup
Furaha na shangwe baada ya kutangazwa mabingwa
****
Timu ya kata ya Ihembe imeibuka mabingwa wa 
Bashungwa Karagwe Cup 2017 baada ya kuifunga Nyaishozi mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Changarawe huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba uliteka hisia za mamia ya  wakazi wa jimbo la Karagwe waliojitokeza kwa wingi.

Ihembe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 25 
kupitia kwa Athumani Chuji aliepiga shuti kali la mpira wa adhabu 
uliomshinda golikipa wa Nyaishozi na kuingia wavuni.

 Bao hilo  lilionekana kuwachanganya Nyaishozi ambao walionyesha kutoelewana katika eneo la ulinzi na kujikuta wakiruhusu bao la pili katika dakika ya 35  lililofungwa na Mshauri Kato aliewatoka walinzi wa Nyaishozi na kufunga 
goli la kiustadi. 

 Kipindi cha pili Nyaishozi waliuanza mchezo kwa kasi 
na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 78 lililofungwa na 
mshambuliaji MC, hata hivyo jitihada za kusawazisha matokeo 
zilikwamishwa na mlinda mlango wa Ihembe alieokoa michomo mingi.


Kufuatia ushindi huo Ihembe walijipatia kombe na 
kiasi cha fedha shilingi milioni moja na nusu huku Nyaishozi wakipata  shilingi laki saba na nusu kama kifuta jasho kwa kushika nafasi ya pili.

Akizungumza baada ya mchezo huo mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent  Bashungwa alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwaka ili  kuibua vipaji vya vijana wa Karagwe waweze kujiajiri kupitia michezo na  kuahidi kuboresha mashindano yajayo kwa kusaka wadau wengine  watakaohakikisha wilaya ya Karagwe inakuwa na timu bora ya kushiriki 
ligi kuu.

Nae kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita ambaye 
pia ni kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime aliyapongeza mashindano hayo na kuahidi mchezo wa kirafiki baina ya Kagera Sugar na kikosi cha  wachezaji bora waliochaguliwa toka mashindano hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments