IGP SIRRO KUMSHUGHULIKIA MANGE KIMAMBI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwanadada Mange Kimambi na kusema kuwa jeshi la polisi linashughulikia suala hilo.


IGP Sirro amesema hayo jana alipokuwa mjini Iringa kwenye ziara ambapo alisema kuwa jeshi la polisi linatambua uvunjifu wa sheria ya makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ambaye amekuwa mkosoaji wa mambo mbalimbali na kutoa machapisho ambayo serikali inaona ni ya matusi na kashfa kwa serikali na viongozi wake.


Aidha IGP Sirro alisema kuwa kwa sasa hawawezi kuweka wazi ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mwanadada huyo ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani


Mbali na hilo IGP Sirro alisema jeshi hilo halitawavumilia maafisa wa polisi na askari wanaowasaidia watu wanaofanya unyanyasaji kwa watoto kwa kuwafanyia vitendo vya ubakaji na ulawiti ili kukwepa mkono wa sheria huku akiwataka wananchi wanaohisi kutotendewa haki katika kushughulikia makosa ya aina hiyo kupeleke malalamiko kwa wakuu wa mikoa na viongozi wengine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments