WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AFUNGUKA TENA KUHUSU TUNDU LISSU

Waziri Ummy Mwalimu amejibu tuhumu zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya serikali baada ya kutaka kuombwa kugharamia matibabu ya Lissu, na kusema kwamba serikali imelazimika kufanya hivyo kwa sababu mgonjwa alijitoa kwenye utaratibu wa serikali.

Ummy Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ametoa maelezo hayo leo kwenye ukurasa wake wa twitter, na kusema kwamba serikali isingeweza kuingilia kati bila kuombwa na familia ya Tundu Lissu, kwani mgonjwa alishatolewa kwenye utaratibu wa serikali kwa kupelekwa Nairobi, na hiyo sio mara ya kwanza kwa serikali kufanya hivyo.

"Mgonjwa alitolewa kwenye utaratibu wa serikali alipopelekwa Nairobi, sasa gharama/tiba zaid yahitajika, serikali inaingiaje bila ridhaa ya familia? Na hii sio mara ya 1 kutokea. Mzee wetu S.Sitta (RIP), alikwenda matibabu London kwa utaratibu binafsi kisha alileta maombi serikali ishiriki", ameandika Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu ameendelea kwa kuandika akisema kwamba mgonjwa ni Mbunge anayehitaji matibabu zaidi, lakini kwa kuwa sasa hivi yupo nje ya utaratibu wa serikali, ili serikali iweze kushiriki ni lazima yawepo maombi ya kufanya hivyo.

Hapo juzi serikali ilitoa tamko ikisema kwamba watakubali kusimamia matibabu ya Tundu Lissu popote duniani iwapo familia yake itaomba kufanya hivyo, na sio vinginevyo, kitendo ambacho kimeibua sintofahamu nyingi kwa baadhi ya wananchi wakiilaumu serikali kwa kutojali matatizo ya Tundu Lissu.
Mgonjwa alitolewa kwenye utaratibu wa Serikali alipopelekwa NRB. Sasa Gharama/Tiba zaid yahitajika.Serikali inaingiaje bila RidhaaYafamilia? 
https:// _/status/911121616024817664 



Mgonjwa ni Mbunge, anahitaji matibabu zaidi. Lkn kwa kuwa sasa yupo nje ya utaratibu wa Serikali, Serikali kushiriki ni lazima yawepo maombi 
https:// _/status/911121616024817664 




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527