WATANZANIA 13 WAFARIKI KWENYE AJALI KAMPALA UGANDA

Watanzania 13 wamefariki na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la biashara Lubanda takribani kilomita 80 kufika kituo cha polisi cha Fika salama karibu na Mto Katonga wilaya ya Mpigi huko Kampala, Uganda.


Ajali hiyo imehusisha gari aina ya fuso yenye namba za usajili UAH 970P na coaster yenye namba T540 DLC waliokuwa wakitumia watu hao wakiwemo watanzania ambao inasemekana walikuwa wakitoka kwenye harusi ya binti wa Dkt. Annette Ibingira ambaye ni mke wa mhazini wa shule ya Wazazi ya Kampala nchini Uganda Dkt. Ibingira.


Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Nkozi pamoja na Double Cure Clinic zilizopo nchini Uganda huku miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo imepelekwa hospitali ya Gombe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi nchini humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527