MBOWE AMSHUKURU MANGE KIMAMBI NA WEMA SEPETU KUHAMASISHA MICHANGO KWA AJILI YA TUNDU LISSU

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewashukuru Watanzania wanaoendelea kumchangia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwataja wanaoongoza katika kuhamasisha uchangiaji mitandaoni akiwamo Mange Kimambi na Wema Sepetu.

Mbowe amesema mpaka leo Ijumaa jumla ya Sh204 milioni zimepatikana katika michango hiyo pamoja na msaada wa hali ambao wamekuwa wakipewa na Watanzania.

“Tunawashukuru wanaoendelea kuchangisha, tunamshukuru Mange Kimambi kwa kuwahamasisha diaspora kuchangia na katika mitandao akishirikiana na Wema Sepetu na wengine,” alisema Mbowe.

Mange alianzisha kampeni ya kumchangia Lissu katika mtandao wa Gofundme akilenga kupata dola za Marekani  50,000 na mpaka kufikia leo saa 10.41 katika mtandao huo kiasi cha dola za Marekani 23,380 ilikuwa imepatikana ambayo ni wastani wa Sh51.3 milioni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527