ASKOFU GWAJIMA AFUTIWA KESI YAKE YA SILAHA


Mahakama imemuachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu katika kesi iliyokuwa inawakabiri ya kushindwa kuhifadhi silaha baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo.

Gwajima na wenzake watatu wamefutiwa mashtaka hayo leo Jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkehe na kuamuru arudishiwe mkoba wake wenye silaha.

Katika kesi hiyo ambayo Gwajima alikuwa akisimamiwa na Wakili Peter Kibatala walishtakiwa hao ambao msaidizi wake Gwajima, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43) na mkazi wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31) mnamo Machi 29 mwaka 2015 walikutwa katika hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A, wakimiliki bastola aina ya Baretta yenye namba CAT 8802 bila kuwa na kibali kutoka mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527