TPB YASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA LILILOANDALIWA NA TSN JIJINI TANGA


Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba
Mashingi akizungumza katika Kongamano la Biashara la Jijini Tanga leo
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba
Mashingi wa pili kutoka kushoto akifurahia jambo na mmoja wa washiriki wa Kongamo hilo la Biashara. 
****


AFISA Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba
Mashingi amewahimiza wafanyabiashara mkoani Tanga kutumia huduma wanazozitoa hususani za mikopo ili waweze kukuza mitaji yao na kutanua wigo wa biashara zao.

Moshingi aliyasema hayo leo wakati akiwasilisha mada katika kongamano la biashara lililofanyika katika Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga na kufunguliwa na Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Dokta Harrison
Mwakyembe.

Kongamano hilo la biashara ambalo limeandaliwa na Tanzania Standard Newspaper (TSN) katika mkoa wa Tanga lilijumuisha wadau kutoka kwenye taasisi binafsi na za serikali,wafanyabiashara wakubwa na wadogo,vijana na wasomi.

“Niwaambie tu huduma hizo zinatolewa na benki yetu kwa ajili ya wafanyabiashara wa aina mbalimbali lakini pia niwapongeze uongozi wa TSN kwa kuandaa kongamano hilo kwa mara nyengine tena katika mkoa wa Tanga”Alisema.

“Lakini pia nawakaribisha wafanyabiashara wote kutembelea tawi letu la hapa mkoani Tanga lililopo mtaa wa Taifa ili muweze kufaidika na huduma mbalimbali tunazozitoa.

Benki yetu ya TPB imejikita kumsaidia mtanzania wa kawaida kuweza kuinua shughuli zake za kiuchumi na hatimaye kukuza uchumi wan chi yetu kwa ujumla ",alisema
Moshingi.

Aidha pia alisema wanaunga mkono juhudi kubwa zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda ikiwemo jitihada za kufufua viwanda vilivyokufa vikiwemo vya mkoani Tanga.

Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutumia fursa za mradi wa bomba la mafuta uliozinduliwa na Rais John 
Magufuli hivi karibuni kuinua biashara zao kwani wao kama benki wapo tayari kuwasaidia kufikia mafanikio hayo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527