MSUKUMA AMLIPUA TUNDU LISU....ADAI ANATAFUTA KIKI TU MAMBO YA BOMBADIER


Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Msukuma amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli hausiki katika sakata la kuvunja mkataba ambao umepelekea ndege ya Tanzania  Bombadier Q-400 Dash 8 kushikiliwa nchini Canada na kusema wapinzani wanatafuta kiki.

Mbunge Msukuma amesema kwa upeo wake jinsi alivyosikiliza upande wa upinzani na majibu ya serikali anaona wazi kuwa ni kweli baadhi ya wapinzani wa nchii hii wanahusika katika kukwamisha jambo hilo kama ambavyo serikali ilivyosema na kudai Rais Magufuli hausiki katika jambo hilo.

"Binafsi yangu naamini kabisa majibu ya serikali kuwa hili suala linauchochezi wa wanasiasa, kwanza vitu vingi walivyosema wapinzani kuhusu sakata hili la ndege ni vya uongo ukianzia lile suala la kuwa Rais Magufuli amekuwa akiiitia hasara serikali hii. 

"Tatizo lililopo mahakamani la kampuni inayodaiwa kuishtaki Tanzania kampuni hiyo imefanya kazi mwaka 1998-99 wakati Magufuli hakuwa Rais wa Tanzania" alisema Mbunge Msukuma

Aidha Mbunge huyo aliendelea kudai jumla ya deni la bilioni 87 ambayo serikali ya Tanzania inadaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd kwa kuvunja mkataba wa kazi halijatokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli.

"Deni hili siyo kwamba limetokana na uongozi wa serikali ya awamu ya tano lakini kama Rais huwezi kukataa deni ambalo serikali inadaiwa akiwa madarakani lakini pia suala hili lipo mahakamani na hatua iliyofikia ni hatua ya mwanzo kabisaa, na si kweli kwamba ndege imekamatwa unaweza kuingia mitandaoni ukaiona ndege ilipo, bado ipo kwao hao Bombadier hivyo Tundu Lissu anaposema ndege imekamatwa siyo kweli.

"Hao watu hao wanaotudai wameenda kufile kesi ya kuzuia mali za Tanzania zisiondoke na serikali inaweza kutoa utetezi wake kwa hiyo hili suala ni kama linawekwa udalali na yote yanafanyika kutokana na umakini wa serikali ya awamu ya tano kwa hiyo wapinzani wanatafuta kiki tu" alisisitiza Msukuma

Siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Agosti serikali ilikiri wazi kuwa ni kweli kuna mgogoro uliopelekea ndege hiyo kushindwa kuingia nchini Tanzania mwezi Julai kama ambavyo ilitangazwa awali na kusema serikali imeanza kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527